Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:38
Mkono wenye nguvu wa jeshi la Iran hautaiacha Israeli / Utawala wa Kizayuni umejiandalia hatima chungu na ya maumivu

Hawza/ Kufuatia jinai ya alfajiri ya leo iliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu pendwa, Hadhrat Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametoa ujumbe kwa taifa kubwa la Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir-Rahmanir-Rahim

Taifa kubwa la Iran!

Utawala wa Kizayuni katika alfajiri ya leo, umeunyoosha mkono wake mchafu na wenye damu na kutenda jinai ndani ya nchi yetu pendwa, na kwa kulenga vituo vya makaazi ya watu, umezidi kuonesha asili yake ovu kuliko hapo awali. Utawala huo unapaswa kungojea adhabu kali.

Mkono wenye nguvu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hautamuacha, kwa idhini ya Allah.

Katika mashambulizi ya adui, baadhi ya makamanda na wanasayansi wamepata shahada. Makaimu wao na wenzao wataendeleza kazi zao bila kusita, inshaAllah.

Utawala wa Kizayuni kwa jinai hii umejiandalia hatima chungu na ya maumivu, na bila shaka utaipokea.

Sayyid Ali Khamenei

1404/3/23 (13 Juni 2025)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha